Macron adai Ufaransa inaiheshimu sana Uturuki

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, amesema,”Tunaheshimu Uturuki na tuko tayari kwa mazungumzo na Uturuki.”
Emmanuel Macron alihudhuria Mkutano Mkuu wa 75 wa Umoja wa Mataifa (UN) uliofanyika kupitia ujumbe wa video kutokana na janga la corona.

Akisisitiza kuwa mazungumzo yenye ufanisi yanahitajika ili kuzuia uwezekano wa mzozo katika Mashariki ya Mediterania na kuheshimu sheria za kimataifa, Emmanuel Macron amekumbusha kwamba wito huu ulitolewa katika Mkutano wa wanachama wa Jumuiya ya Ulaya (EU) , Mkutano wa Nchi za Kusini mwa Ulaya uliofanyika Corsica.

Macron aliongeza kwa kusema,

“Tunaiheshimu Uturuki na tuko tayari kufanya mazungumzo nayo. /…/ Sisi watu wa Ulaya, tuko tayari kwa mazungumzo.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *