Maafisa ushirika nchini waonywa kuwadidimiza wakulima

Serikali imewataka maafisa ushirika  katika halmashauri zote nchini kusimamia kikamilifu   vyama vya Msingi kwa kutoa ushauri wenye tija badala ya kuwadidimiza wakulima na kusababisha  hasara kubwa kwa wakulima na serikali kwa ujumla.

Kauli hiyo imetolewa jana na mwenyekiti wa tume ya maendeleo ya ushirika nchini (TCDS) Dokta. Titus  Kamani kwenye mkutano mkuu wapili wa chama kikuu cha ushirika mbogwe na bukombe (MBCU) kilichofanyika katika wilaya ya Mbogwe mkoani Geita.

Amesema  Serikali imeibosha Sheria ya Ushirika  na  kwamba kwa sasa usimamizi na matumizi ya mali za vyama vya msingi na Ushirika  vinasimamiwa na  Maafisa Ushirika wa kila wilaya hivyo serikali haitegemei kuona hasara unaotokana na upoptevu wa mali mbalimbali vya vyama vya Msingi.

Mkuu wa wilaya ya mbogwe MATHA  MKUPASI amesema mwaka huu wakulima watazalisha kwa wingi  baada ya kupata pembejeo kwa wakati kutoka kwa  kampuni ya  Petrobena  inayojihusisha na  masuala ya pembejeo kwa wakulima Kuondoa urasimu ulikuwepo hapo awali.

Mmoja wa wakulima wa Tambaku CATHERIN AGUSTINO ameziomba taasisi za fedha kuacha ubaguzi katika utoaji wa mikopo kwa baadhi ya amcos huku Samwel Madaraka afisa kilimo na ushirika wilaya ya mbogwe, akiwataka wakulima kutumia pembejeo bora ambazo haziharibu ardhi.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *