LIVERPOOL NGUMU KUTETEA UBINGWA.

 


LEGENDI, Jamie Carragher anaamini kwamba Klabu yake ya zamani ya Liverpool itapata tabu kubwa kutetea taji la ubingwa wa Ligi Kuu England bila uwepo wa beki kisiki Virgil Van Dijk.

Beki huyo wa zamani wa Liverpool amesema kuwa kwa sasa Jurgen Klopp anapaswa afaye usajili mkubwa kwa kumvuta Dayot Upamecano beki wa kati anayecheza ndani ya RB Leipzing ili awe mbadala wa Dijk kwenye usajili wa mwezi Januari.

Dijk kwa sasa anatibu jeraha lake la goti alilolipata kwenye mchezo wa Ligi Kuu England wakati timu yake ilipokuwa ikipambana na Everton kwenye sare ya kufungana mabao 2-2 baada ya kupata changamoto kutoka kwa kipa wa timu hiyo Jordan Pickford alipokuwa akimzuia asifunge.

Kutokana na majeraha hayo upo uwezekano mkubwa wa beki huyo mhimili ndani ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England kukosa mechi zote za msimu huu akiuguza jeraha hilo. Carragher aliyecheza mechi 508 ndani ya Liverpool na kufunga mabao manne  msimu wa 1996-2013 amesema kuwa itakuwa ngumu kwa timu hiyo kutetea ubingwa.

“Ninadhani kwamba van Dijk alikuwa fiti kwa msimu uliopita na timu iliweza kushinda taji la Ligi Kuu Engalnd, kwa wakati huu bila uwepo wake ndani ya kikosi kutakuwa na ugumu mkubwa, ni lazima Klopp afanye usajili kwa mwezi Januari ili kuongeza nguvu ndani ya kikosi,” amesema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *