Ligi kuu soka Zanzibar kuanza bila mashabiki

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ)   imetoa utaratibu wa  namna ya kumaliza ligi kuu soka ya Zanzibar msimu wa mwaka  2019/2020 ambapo Michezo iliyosalia italazimika kuchezwa katika kituo kimoja Cha Unguja na  viwanja vitakavyo tumika ni  viwanja viwli, kiwanja Cha Amani stadium na Mao Tse Tung.

Ligi kuu soka Zanzibar ililazimika kusimama kwa muda kufuatia mripuko wa maradhi ya homa kali ya mapafu (COVID 19) yanayosababishwa na virusi hatari vya Corona ambavyo vimeikumba Duniani kote.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisi kwake Migombni Mjini Unguja, Katibu Mkuu wa Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Zanzibar,Omar Hassan  kingi alisema kwamba ligi kuu soka Zanzibar  inapaswa kuendelea kuchezwa kama maagizo yaliyotolewa na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kufunguliwa kwa michezo, hivyo ligi kuu italazimiaka itachezwa kwa kituo kimoja tu cha Ungja.

Alisema  kwamba uwamuzi wa kichezeka michezo iliyosalia katika kituo kimoja itasaidia kuepuka gharama za uendeshaji wa ligi hiyo kwa michezo michache ilyobakia.

Pia Alisema uwamuzi huo umezingatia kanuni mbalimbali na uongozo wa Afya ambapo viwanja vitakavyotumika ni viwanja vya Amani Staduim na kiwanja cha Mao Tse Tungu kwa michezo ambayo imesaia huku michezo ya mwanzo itachezwa bila ya mashabiki kuingia uwanja

“Kwa hatua hii ya mwanzo michezo itakayotechwa bila ya mashabiki kuingia viwanjani, washabiki wa timu husika wanatakiwa kufuatilia michezo kwa Televion zitakazo onesha pamoja na redio zitakazo tangaza matukio michezo hiyo” alisema Kingi.

Aidha alisema kwamba viongozi wote wa ZFF pamoja na wadau wa michezo watakao ingia viwanjani wanapaswa kufuata utaratibu muongozo unaotolewa na wataalaumu wa afya kwa kunawa mikono na kupaka sanitaiza vitakasa mikono.

“Jambo la saba viongozi wote wa vilabu, marefa, ZFF na watu wote ambao wataingia katika shughuli za michezo wanawe mikono kwa sababuni au kutumia sabuni, jambo hili tunauwezo nao, lakini watu wote wanapaswa kukaa mitaa moja moja kwa benchi la ufundi na wadau wengne ili kujikinga kuambukiza virusi hivyo vya Corona” alisema Kingi.

Hata hivyo alisema wakati michezo ikiwa inaendela wataalamu wa Afya kupitia wizara ya afya watakuwa wanatoa elimu mbalimbali ya namna ya  kuepuka kuenea kwa virusi hivyo michezoni.

“Elimu mbalimbali itatolewa wakati michezo ikiendelea kwa njia ya vipeperushi na njia nyinginezo ili kuepusha namna ya kuenea wa vurusi hivi, ambapo wataalamu wa Afya watapita kwa madaktari wa timu hizi na kuwapa Elimu ya kujikinga” alisema Katibu Kingi.

Aidha aliagiza kkila kiwanja kitakachotumika kwa mazoezi na mechi kuwekwe chumba maalumu ambacho kitakuwa kinatumka kwa ajili wale wagonjwa ambao watashukiwa kuwa na dalili za ugonjwa huo.

“Tunaagiza kwamba kila kiwanja kitengwe chumba kimoja ambacho kitatumka kwa ajili ya kuwaweka wagonjwa mbao wanashukiwa na ugonjwa huo au watenge sehmu yoyote ambayo inaweza kutumika kwa ajili hiyo sambamba na hayo kila kiwanja kinapaswa kuwe na gari la kubebea wagonjwa” alieleza Katibu Kingi.

Ligi Kuu Soka ya Zanzibar ina jumla ya timu 16 zikiwemo 11 kutoka Kisiwani Unguja na 5 kutoka Kisiwani Pemba ambapo michezo huchezwa kwavituo viwili kituob cha Unguja na kituo cha Pemba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *