Kuwakana walimu ni kuikana nafsi yangu siwezi kuwatupa- Rais Magufuli

“Siwezi kuwatupa walimu, tunajenga nyumba moja, mimi nilikuwa mwalimu, kuwakana walimu ni kuikana nafsi yangu siwezi kuwatupa, naamini hata kama uongozi huu hautochaguliwa, huo uongozi ujao pia utajenga uhusiano mzuri na Serikali”-JPM

“Nilipotangaza kufunga vyuo na shule kupisha corona, kesho yake nikapigiwa simu na Rais wa CWT, akaniambia usifanye kama Nchi nyingine ukakata mishahara ya walimu, nikatafakari, nikasema corona hata ikikikaa miaka 10 sitokosa mshahara wa kuwalipa walimu”-JPM

“Kwenye huu uchaguzi chagueni Viongozi wenye uchungu na walimu, epukeni kuchaguana kwa kujuana au kwa rushwa, mtakaochaguliwa muwatumikie walimu sio kwa maslahi yenu binafsi” -JPM

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *