KUTOPIGA KURA NI SAWA NA KURUHUSU USHINDI KWA VIONGOZI WASIOKUWA NA SIFA

MAKALA

Na Salvatory Ntandu

Uchaguzi wa serikali za Mitaa nchini Tanzania hufanyika kila baada ya miaka minne ambapo wananchi katika eneo lote la Tanzania bara na visiwani hutimiza haki yao ya kikatiba ya kuchagua na kuchaguliwa kuwa viongozi katika mitaa,vijiji,sheia na vitongoji mbalimbali hapa nchini.

Msomaji Makala hii inajikita zaidi kuangazia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu Noveba 24 mwaka huu ambapo vyama mbalimbali vya siasa vitachuana kuwania nafasi za uongozi likiwa ni takwa la kisheria na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyoelekeza kuwa uchanguzi huo kufanyiaka kila baada ya miaka mnne.

Katika Uchaguzi wa serikali za mitaa nafasi zinazowaniwa huwa ni Mwenyekiti wa kijiji/Mtaa,Kitongoji,balozi wa nyumba kumi na wajumbe wa halmashauri ya kijiji au mtaa ambao wote kwa pamoja hutokana na vyama vya siasa.
Uchaguzi huu huwa ni maandalizi ya Uchaguzi mkuu ambapo wananchi huweza kuwachagua viongozi wao ambao watabeba dhima ya kuwagongoza kwa muda wa miaka minne sambamba na kuhakikisha Maslahi ya wananchi yanalindwa na jamii inakuwa na amani.

Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo, ndiye mwenye jukumu la kusimamia uchaguzi huu ambapo kwa mwaka huu utafanyika Novemba 24, 2019.

kumekuwepo na dhana potofu katika jamii kwa baadhi ya watu kwenye jamii kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa hauna maana yeyote na kupiga kura ni sawa na kupoteza muda wako bure na wengine husubutu kusema viongozi hao hawana maanufaa yeyeote kwenye jamii kitu ambacho hakina ukweli.

Serikali ya mitaa/kijiji ipo kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na inamamlaka kamili kwa kuwa na safu za uongozi zinazoheshimika na kutoa maamuzi ambayo hayawezi kuingiliwa na mamlaka zingine ikiwa yamefanyika kwa kungatia haki na ustawi wa jamii husika.

Yapo maeneo mbalimbali hapa nchini ambayo viongozi wa serikali za mitaa zimefanya vizuri katika usimamizi wa miradi ya maendeleo na jamii kunufaika na uwepo wa miradi hiyo mfano ujenzi wa Shule,zahanati,Visima,barabara,na madaraja ambayo huibuliwa na wananchi kupitia mikutano yao ya vijiji na mitaa.
Binafsi naamini Tujikita zaidi katika kutoa elimu ya Mpiga kura wananchi itawapa hamasa ya kutambua umuhimu wa uchaguzi huu husasani wale ambao wapo katika maeneo ya vijijini ambao huenda ni wakulima na wafugaji ambao hawelewi maana ya uchaguzi wa serikali za mitaa.

Kutokwenda kupiga kura inaweza ikasababisha watu wasio kuwa na sifa kutumia nafasi hiyo kuwa viongozi kwa mfano kura moja tu inatosha kumpa ushindi kiongozi endapo watu wasipojitokeza katika kupiga kura kwa wingi kwa kigezo cha kususia uchaguzi au kudhani kuwa wanapoteza muda dhana hii potofu imekuwa inajitokeza husasani mjini na vijiji.

Palipo na mafanikio dosari halikosekani mathalani katika uchaguzi wa serikali za mitaa sheria na taratibu za kuwapata wagombea katika nafasi hizi zisipozingatiwa zinaweza kusababisha vurugu katika uchaguzi au kuwakatisha tama wananchi kujitokeza kushiriki katika uchaguzi na kusababisha wagombea wasiokuwa na sifa kuchaguliwa.

Kwa mfano katika halmashauri ya Mji wa kahama mkoani Shinyanga katika Mtaa wa Mbulu mission mwaka 2014 kuliibuka vurugu katika chumba cha kuhesabia kura za mwenyekiti wa serikali ya mtaa, vurugu hizo zilisababisha kuchomwa moto kwa kituo hicho na karatasi za matokeo kuwaka moto na kusababisha wananchi wa mtaa huo kukosa mwakilishi kwa muda wa miaka minne.

Hebu tutafakari kidogo, wananchi wa mtaa huu wamekosa wawikilishi kwa muda gani na je Tamisemi ambao ndio wanadhima ya kusimamia uchaguzi huu wamejipangaje kuhakikisha dosari hizi hazitokezi tena na wananchi kama hawa ambao wamekosa viongozi wao kwa muda mrefu wanawahakikishiaje usalama wao katika kipindi cha uchaguzi wa serikali wa mwaka huu.

Elimu ya mpiga kura inahitajika zaidi hasa katika maeneo ambayo yalibainika kwa na changamoto katika chaguzi mbambalimbali hapa nchini hususani maafisa uchaguzi na asasi za kiraia kuwaelewesha wananchi juu ya umuhimu wa kupiga kura na kuwa chagua viongozi bora tena wenye sifa ili waweze kusimamia maendeleo yao.

Kwa mujibu wa Afisa Uchaguzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Elikana Shija alisema maandalizi yote ya uchaguzi huo yamekamilika huku elimu ya mpiga kura inaendelea kutolewa kwa wananchi njia mbalimbali ikiwemo mikutani na vyombo vya habari kama vile radio na Televisheni.

Kanuni za uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa ngazi ya vijiji, vitongoji na mtaa za mwaka 2019 nchini Tanzania zimeainisha aina nane za vitambulisho ambavyo msimamizi wa kituo cha uchaguzi anaweza kumtaka mpiga kura aonyeshe ili kujiridhisha na jina kama ndilo liko katika orodha ya mpiga kura.

Kanuni hizo zimetaja vitambulisho hivyo ni kitambulisho cha mpiga kura, cha kazi, hati ya kusafiria, kadi ya bima ya afya, cha shule au chuo, mfuko wa hifadhi ya jamii, leseni ya udereva na kitambulisho cha Taifa.

Kanuni hiyo ya 33 kifungu cha pili kinasema, “Msimamizi wa kituo anaweza kumtaka mpiga kura aonyeshe kitambulisho kitakachoonesha kuwa jina la mpiga kura huyo ndio lililomo kwenye orodha ya wapiga kura.”Alisema Jafo.

Kwa mujibu wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo amsema upigaji kura utaanza saa 2.00 asubuhi na kuhitimishwa saa 12.00 jioni na waangalizi wa uchaguzi wataruhusiwa baada ya kupata kibali kutoka kwa katibu mkuu Tamisemi na maombi yatatakiwa kupata kibali kwa katiba mkuu ndani ya siku 21 baada ya tangazo la uchaguzi kutoka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *