KOCHA SIMBA HANA CHAGUO LA KWANZA

KOCHA Mkuu wa Simba, Mbelgiji, Sven Vandenbroeck, amewachambua washambuliaji wake wote, huku akidai kuwa bado hana chaguo la kwanza na kudai kwamba atawatumia kulingana na michezo husika.

Simba kwa sasa ina washambuliaji wa kati wanne ambao ni Meddie Kagere, John Bocco, Chris Mugalu na Charles Ilanfya ambao kwa pamoja wameifungia timu hiyo mabao 10 katika michezo ya Ligi Kuu Bara kabla ya mchezo dhidi ya Kagera Sugar.

Akizungumza na Spoti Xtra, Sven alisema mpaka sasa hana mshambuliaji tegemeo au chaguo la kwanza katika kikosi chake ila hupenda kuwatumia washambuliaji hao kulingana na aina ya wapinzani ambao hukutana nao.

“Siwezi kusema kuwa chaguo langu namba moja ni nani, ila kinachotakiwa kufahamika kuwa wote ni washambuliaji wangu na nitawatumia kulingana na aina ya mechi ambayo ipo mbele yetu.

“Wote ni washambuliaji wazuri, ukiwaangalia wanavyocheza utagundua kuwa ni wachezaji wa aina gani, tunafurahia kuwa na washambuliaji wa aina yao na naamini wataisaidia timu kupata mafanikio zaidi,” alisema kocha huyo.

Kesho ana kibarua cha kusaka pointi tatu kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Yanga utakaochezwa Uwanja wa Mkapa saa 11:00 jioni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *