KLOPP HAELEWI CHA KUFANYA KUHUSU NAFASI YA ULINZI

JURGEN Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool kwa sasa yupo kwenye wakati mgumu kuhusu uimara wa safu yake ya ulinzi baada ya beki wake mwingine Fabinho Tavares kuumia kwenye kipindi cha kwanza wakati wakipambana na Midtylland usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Anfield.

Raia huyo wa Brazili alikuwa anaziba nafasi iliyokuwa inachezwa na beki kisiki wa timu hiyo Virgil van Dijk akisaidiana na Joe Gomez kwa kuwa Dijk huenda ataukosa msimu mzima kwa kuwa anatibu jeraha la goti.

Kwenye mchezo huo Liverpool ilishinda mabao 2-0 ambapo bao la kwanza lilipachikwa na Diogo Jota dakika ya 53 na Mohamed Salah dakika ya 90+3 kwa mkwaju wa penalti.

Liverpool ambao ni mabingwa watetezi wana kazi kubwa ya kufanya kwenye safu ya ulinzi kutokana na mwendo wao ulivyo pamoja na ushindani ambao umeanza kuwa mkali kwa msimu wa 2020/21.

Klopp amesema kuwa ana kazi kubwa kwa msimu huu jambo ambalo linamfanya asijue la kufanya kwa sasa kwa kuwa mambo sio mazuri kwake.

“Hakika kwa sasa ambacho ninakijua hata sielewi namna mambo ambavyo yanakwenda labda baadaye nitajua cha kufanya ila kiukweli hali sio nzuri kwa sasa.

“Tusubiri na tuone kwa kuwa ameniambia kwamba hajiskii vizuri ila tutajua mambo yatakavyokuwa hapo baadaye lakini ukweli mambo sio mazuri,unapozungumzia maumivu ya misuli najua jinsi iilivyo ila huwezi kutoa taarifa kamili ikiwa hujapata ripoti,” amesema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *