Kiwanda cha Ushonaji cha wana mama wa Ki-Badhi Chazinduliwa Isaka Kahama,Jumuiya ya Kiislamu ya Istiquaama yashusha neema.

Wanawake mafundi Cherehani katika mji wa Isaka Wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameishukuru jumuiya ya Internatioanl istiqumaa Muslim Community  ya nchini Oman kwa kuwapa msaada ya Vyerehani hali itakayowafanya waondokane  kushona kwa kutumia Vyerehani vya kukodi.

Wakiongea mara baada ya kukabidhiwa vyerehani hivyo wanawake hao wamesema kuwa walikuwa hawana uwezo wa kununua vyerehani   na kwamba kwasasa wataweza kujisimamia na kujikimu katika maswala mbali mbali ya Familia.

Katika hatua nyingine wanawake hao wameomba wafadhili wengine kujitokeza kuwapa msaada wa vitambaa,kwani kiwanda chao ni kipya na hakina uwezo wa kununua malighafi kama majola ya vitambaa ili kujiendesha.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Isaka Rajab Kaombwe   ameishukuru  jumuiya hiyo kwa msaada wa Vyerehani hivyo na kuwaomba wafadhili kufikisha mradi huo katika maeneo mbalimbali huku akiwataka wanawake wa Isaka kutunza Vyerehani hivyo.

Awali akikabidhi Vyerehani hivyo kwa niaba ya Wafadhili Mzee wa Kii-badhi kutoka Halmashauri ya Mji wa Kahama Mohamed Malik amewataka wanawake hao kuzitunza Cherehani hizo na kuwa wamoja  na kuwataka kupeleka cherehani zingine katika vijiji jirani ili kuufanya mradi huo uwe mkubwa.

Jumuiya ya Internatioanl istiqumaa Muslim Community  ya nchini Oman imeendelea kuunga mkono Juhudi za Serikali ya awamu ya Tano ya kukuza uchumi wa Viwanda kwa kutoa Msaada wa Vyerehani 15 na jengo la ushonaji vyote vikiwa na gharama ya Shilingi milioni 15 za kitanzania kwa ajili ya kufungua kiwanda cha Ushonaji kwa wanawake wa Kijiji cha Isaka halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *