Kilo milioni 52 za korosho ghafi zauzwa katika minada.

Dodoma. Jumla ya kilo 52,748,740 za korosho ghafi zenye thamani Sh136.76 bilioni  zimeuzwa katika mnada ya korosho nchini.

Akizungumza leo Jumapili Novemba 16 2019 Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga amesema kiasi hicho tangu minada hiyo ilipoanza Oktoba 31 2019.

Amesema jumla ya makampuni ya ununuzi yaliyosajiliwa hadi kufikia Novemba 10 mwaka huu yalikuwa ni 85 lakini ni makampuni 48 ndio yaliyopewa leseni baada ya kutimiza vigezo vyote.

“Kumekuwa na mwenendo mzuri tangu kuanza kwa minada ya wazi. Idadi ya wanunuzi wanajitokeza kutaka kununua korosho ni kubwa,” amesema.

Amesema bei zimeendelea kupanda kutokana na mahitaji makubwa ya korosho.

Amesema bei imepanda kutoka Sh 2409 na Sh 2559 hadi kufikia kati ya Sh 2677 hadi Sh2727 kwa kilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *