Kikongwe chenye miaka bilioni 1.5 chagundulika

Wanasayansi waligundua vumbi lililokuwa katika kimondo hicho kilichodondoka duniani mwaka 1960 kuwa kina umri upatao bilioni 7.5.

Ukongwe wa vumbi hilo ililojitengeneza katika nyota inawezekana kuwa ina muda mrefu zaidi ya mfumo wa sola ulipoanzishwa.

Kundi la watafiti hao wameelezea matokeo ya utafiti wao katika jarida la kitaifa la mafunzo ya Sayansi.

Wakati nyota hiyo ilipoanguka, vipande ambavyo vilitengenezewa huwa vinasambaratika hewani, chembechembe zake uweza kuunda nyota mpya, mwezi au kimondo.

Kikundi cha watafiti kutoka Marekani na Switzerland wamefafanua kuwa chembechembe 40 walizozifanyia kazi zimeweza kuwa sehemu ya kimondo kilichoanguka mwaka 1969.

“Huanza kwa kusagwa kwa kimondo hiko kuwa kama poda,” alisema mtafiti Jennika kutoka sehemu ya makumbusho na chuo kikuu cha Chicago.

“Wakati ambao vipande vyote vimetengana, kuna namna ambayo isiyo ya kawaida huwa inajiunga na kunukia kama siagi ya karanga.”

Huwa inabadilika kuwa tindikali, na kuacha vumbi la nyota tu.

“Ni sawa na kutafuta sindano katika majivu,” alisema Philipp Heck.

Namna ambavyo wanasayansi walivyobaini ukongwe wa sehemu hiyo ya kimondo.

Baadhi ya sehemu za kimondo hicho zilikuwa zimejichanganya na chembechembe mpya.

Watafiti walitumia mfumo wa ‘isotope’ kugundua tarehe ya sehemu hiyo ya kimondo.

Wanasayansi wametumia njia nyingi kuweza kuhakiki utafiti wao na kubaidi kama mionzi ya sehemu hiyo ni ya muda gani?

Baadhi ya sehemu iligundulika kuwa kongwe zaidi tofauti na sehemu nyingine ya kimondo.

Ilionyesha kuwa ni kama ina muda wa bilioni 4.6-4.9 .

Ukilinganisha na jua ambalo lina muda wa bilioni 4.6 billion na dunia ni bilioni 4.5.

Ingawa sehemu ya vumbi lake inatajwa kuwa na umri wa miaka bilioni 7.5 .

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *