Kigogo C C M kahama amiliki danguro

Mkuu wa wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, ANAMRINGI MACHA  amefanya ziara ya kushtukiza  katika baa ya Bijampola iliyoko Mtaa wa Nyihogo mjini Kahama na kukuta nyumba bubu ya kulala wageni ambayo inatumiwa  kama danguro la wanawake wanaofanya biashara haramu ya Ngono.

Akizungumza na wanawake aliowakuta katika vyumba ya baa hiyo, MACHA ameshangazwa na hali ya vyumba hivyo kuwa vichafu huku vikitoa harufu mbaya, huku akilazimika kumpigia simu mmiliki wa Baa hiyo, SPILAUS BIJAMPOLA  na kumtaka  azingatie usafi ndani na nje  ya nyumba yake.

Katika hatua nyingine, MACHA amezitaka mamlaka zinazohusika kwenda kutembelea nyumba hiyo ya kulala wageni ili kujiridhisha na uhalali wake kibiashara na kwamba wachukue hatua za haraka kwa kuwa  mazingira ya nyumba hiyo yanahatarisha afya za watu.

Akizungumza kwa Njia ya Simu mmliki wa baa hiyo  BIJAMPOLA amesema nyumba hiyo kwa sasa haitumikwa kwa leseni ya biashara  ya kulala wageni bali  kila chumba ameweka mpangaji na kwamba jukumu la kusafisha chumba si lake bali ni la mpangaji  anayelala katika chumba  hicho.

 

Biashara haramu ya Ngono imeshamiri katika mji wa Kahama hususan maeneo yenye mkusanyiko mkubwa wa watu nyakati za usiku, licha ya mamlaka husika kukemea vitendo hivyo mara kwa mara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *