Kaya masikini Kahama zapewa darasa kuhusu Mpango wa kuweka akiba na kukuza uchumi pasipo kutegemea Tasaf.

Kaya masikini zilizo kwenye mpango wa kunusuru kaya masikii katika halmashauri ya mji wa kahama mkoani shinyanga zimetakiwa kutumia fursa walioipata ya mradi wa mpango wa uweka akiba na kukuza uchumi wa kaya kwa lengo lakutokuwa tegemezi tena endapo TASAF itaondoka.

Kauli hiyo imetolewa na mratibu wa TASAF halmashauri ya mji wa kahama LEORAD NCHINJAYI wakati akizungumza na walengwa hao katika kijiji cha bumbiti katika kata ya mondo wakati wa kuunda vikundi hivyo ambayo vitawasaidia katika maisha yao ya baadae.

NCHINJAYI amesema lengo la mradi huo ni kuziwezesha kaya masikini kufikia na kupata huduma za mitaji, masoko, ujuzi wa kazi na ajira, pamoja kuwezesha vikundi vya kuweka akiba na kuwekeza kuunganishwa na taasisi za fedha.

Kwa upande wao walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya masikini katika kijiji cha Bumbiti katika kata ya Mondo wamesema kabla ya TASAF kuja walikuwa na hali ngumu ambapo walikuwa wakipata mlo moja na kwa sasa kupitia TASAF wameweza kujenga nyumba na kusomesha watoto wao.

Naye wake mjumbe wa TASAF kutoka Bumbiti ESTA JOHN amesema kuwa tangu kuja kwa mpango wa kunusuru kaya masikin TASAF katika kijiji hicho walengwa wameweza kunufaika kwa kupata milo mitatu kuwa na miradi ya kilimo, ufugaji, kujenga nyumba na kusomesha watoto wao.

Hata hivyo, kwa awamu ya TASAF kwa sasa inatekeleza mpango wa kuweka akiba na kukuza uchumi wa kaya chini wa mpango kunusuru kaya masikni kwa lengo la kuwawezesha kufikia fursa ya kujiunga na vyombo rasmi vya fedha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *