Kauli ya Majaliwa baada ya kuteuliwa tena kuwa waziri mkuu

Waziri Mkuu mteulu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema kupendekezwa kwake kwa mara nyingine tena kuwa Waziri mkuu wa Tanzania na Rais John Pombe Magufuli si jambo dogo huku akimshukuru kwa kumpendekeza kwa mara nyingine tena.
Akizungumza mara baada ya kupendekezwa na kuidhinishwa na wabunge wa bunge la 12 kupitia upigaji kura uliofanyika leo bungeni, Dodoma, Majaliwa amewashukuru wabunge wote kwa kumpigia kura nakuwahakikishia kuwa watafanya kazi pamoja.

“Jambo hili si dogo, namshukuru sana kwa imani yake kubwa aliyonayo juu yangu nakuendelea kuniamini kwamba naweza kufanya niliyofanya katika kipindi cha miaka mitano na zaidi katika kipindi kingine kijacho” amesema Majaliwa

Majaliwa ameongeza pia,”Niendelee kumhakikishia kwamba matamanio yake yaliyompelekea kutoa jina hilo kulileta mbele ya bunge hili tukufu ambayo anaamini na wabunge wenzangu kwa namna ambavyo mmepiga kura nyingine ni namna tosha mheshimiwa rais ameleta jina ambalo mnaamini nitamsaidia kazi, nami niwahakikishie nitafanya hivyo”

Leo Rais Magufuli amempendekeza mbunge wa Ruangwa Kassim Majaliwa kuwa waziri mkuu wa Tanzania kwa muhula mwingine tena huku wabunge wakimpigia kura zakutosha kuonyesha kuridhishwa na pendekezo hilo la Rais lililowasilishwa na mpambe wake bungeni Dodoma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *