Katwila amwaga wino IHEFU

IMEELEZWA kuwa, Zuber Katwila, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar amebwagwa manyanga kutokana na timu hiyo kuwa na matokeo ya kusuasua kwa msimu wa 2020/21.

Katwila ambaye alikuwa mchezaji wa zamani wa timu hiyo na alikuwa nahodha kwa sasa hayupo na timu kambini Morogoro ikiwa kwenye maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo FC, unaotarajiwa kuchezwa kesho Oktoba 19.

Mchezo huo utakuwa ni wa saba kwa Mtibwa Sugar baada ya kucheza mechi sita na imepoteza mechi tatu na kushinda moja huku ikiambulia sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Simba, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa hakuna taarifa rasmi waliyoipata kuhusu Katwila licha ya kuwepo kwa tetesi kwamba amejiuzulu.

“Kweli ninaskia tetesi kuhusu suala hilo ila mpaka sasa halijawa rasmi kwani hakuna taarifa kutoka kwa uongozi pamoja na yeye mwenyewe ambayo nimeipata ila ngoja kwanza tumalize mchezo wetu dhidi ya Namungo hapo nitakaa na uongozi ili kutambua ukweli.

“Kwa sasa Katwila hayupo na timu Morogoro yeye alimpa taarifa kocha msaidizi, Vincent Barnaba ambaye anasimamia timu kwa sasa, anasema kuwa alipata dharula kwani mara ya mwisho tulikuwa naye baada ya kupoteza mbele ya Biashara United, Mara.

“Ikitokea ikawa hivyo basi tutaweka kila sawa kwani wengi wanaipenda Mtibwa Sugar hata mimi ninajua kwamba kuna Watanzania zaidi ya milioni moja ambao wanauwezo mkubwa,” amesema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *