Katibu Mkuu CWT: Tunashukuru Rais kwa kuruhusu walimu kulipwa mishahara tukiwa nyumbani wakati huu wa ugonjwa wa Corona

“Jumla ya wajumbe 1138 wameshiriki katika mkutano huu kutoka Mikoa 26 ya Tanzania Bara kwa ajili ya uchaguzi wa Viongozi wa Kitaifa wa Chama cha Walimu watakaoongoza kwa miaka mitano kuanzia mwaka 2020”-Katibu Mkuu CWT, Deus Seif mbele ya JPM Dodoma

“Tunashukuru Rais Magufuli kwa tamko lako la kuruhusu walimu kuendelea kulipwa mishahara tukiwa nyumbani wakati huu wa ugonjwa wa Corona” – Katibu Mkuu CWT, Deus Seif mbele ya JPM

“Chama cha Walimu Tanzania kinatambua jitihada kubwa ambazo zinafanywa na Serikali hii katika kuboresha maisha ya watanzania wakiwemo walimu, tunakupongeza pia kwa kuboresha Sekta ya Elimu – Katibu Mkuu wa CWT, Deus Seif mbele ya JPM

“CWT tunakupongeza kwa kuhakikisha miundombinu na thamani inapatikana katika mazingira ya kufundishia na kujifunzia, upandishaji wa madaraja pamoja na urekebishaji wa mishahara”- Katibu Mkuu CWT, Deus Seif mbele ya JPM

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *