Kanye West achangia bilioni 4.6 kumsomesha mtoto wa George Floyd

Ikiwa ni masaa machache baada ya kutangazwa na Forbes kuingiza kiasi cha Tsh Bilioni 393.8 kwa mwaka 2020, na kuwa kinara kwa wasanii, Kanye West kwenye headline kwa mara nyingine.

Kanye ameripotiwa kuchangia kiasi cha $2M ambazo sawa na takribani Tsh. Bilioni 4.6 kwenye familia za George Floyd, Breonna Taylor na Ahmaud Arbery.

Kwa mujibu wa taarifa, pesa hiyo yote imeenda kuchangia mfuko wa hifadhi ya fedha kwa ajili ya masomo uitwao ‘529 College Savings Plan’ ili kumsaidia binti wa marehemu George Floyd, Gianna (6) kulipa ada ya shule.

Mbali na hilo, Kanye pia amechangia na gharama za kuendesha kesi, kwa familia hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *