????????????????????????????????????

Kampuni ya Petrobena yatajwa kuongeza uzalishaji wa Tumbaku katika chama cha Milambo Mkoani Tabora.

WAKULIMA wa zao la tumbaku  wa chama kikuu cha ushirika  cha Milambo kilichopo wilayani Urambo Mkoani Tabora wameipongeza Kampuni ya usambazaji pembejeo ya Petrobena kwa kuwarahisishia upatikanaji wa mbolea na madawa hali ambayo imesababisha kuongeza uzalishaji wa zao hilo katika msimu wa 2019/2020.

Hayo yamebainishwa  na baadhi ya wakulima wa chama hicho Abisai Kasenge Zacharia William na Mathew Luzagila ,katika kikao cha Mkutano Mkuu wa pili mkuatano amabo umeafanyika katika ukumbi wa kanisa katoliki wilayani Urambo.

Wamesema  kuwa msimu uliopita wamepata mafanikio makubwa ya zao hilo kutokana na kampuni ya Petrobena kusambaza  pembejeo za mbolea na Madawa ya Mimea kwa wakati katika vyama vyao.

Wameongeza kuwa  kabla ya kuwepo kwa kampuni ya Petrobena wakulima  wengi walikuwa wakipata shida kucheleweshewa  pembejeo za mbolea na madawa hali ambayo ilikuwa ikifanya zao lao la  Tumbaku kuharibika

Aidha Wakulima hao wamewataka mawakala wengine wa usambazaji pembejeo kuwa waaminifu kwa kuiga mwenendo wa kampuni ya Petrobena  ili kuweza kumsaidia mkulima wa zao la Tumbaku kuzalisha kwa wingi zao hilo

Hata hivyo  Wakulima hao  wameongeza kwa kusema  kuwa Petrobena mbali ya kuwa  wakala wa usambaji pembejeo na Madawa ya  mimea wameiomba  kampuni hiyo kufikiria  kuwa miongoni mwa makapuni ya ununuzi wa tumbaku hapa nchini kutokana na uwezo wao, weledi mkubwa na kujali maslahi ya mkulima wa tumbaku.

Nae Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika wa wakulima wa tumbaku  cha Milambo  Hassan Magola amesema dhamira ya chama hicho ni kuendelea kutetea na kusimamia haki za wakulima wake ili wainuke kiuchumi.

Kaimu Mrajisi wa Vyama wa Ushirika Tanzania Benson Mlyege amewataka    viongozi wa vyama vya ushirika kuwa waaminifu na kuwasilisha taarifa ya mali za vyama vyao, thamani ya mali hizo na mahali zilipo ili kuepuka ubadhirifu na wizi katika vyama vya ushirika .

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania Titus Kamani, amevitaka vyama vya ushirika hapa nchini  kuhakikisha viongozi wa vyama vya msingi na wakulima wanapewa elimu ya ushirika na kilimo bora ili kufanya kilimo kiwe na tija katika maeneo yao.

Kamani amewaonya viongozi wa vyama vya ushirika wanaotaka kujitajirisha haraka kupitia jasho la mkulima kuacha mara moja tabia hiyo huku Akiwatahadrisha  wale wasioridhika na hali zao kujiondoa mara moja katika vyama hivyo kabla hawajaondolewa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *