Kampuni ya kichina yatoa milioni 10 kuunga mkono Serikali mapambano ya Covid 19

Mkuu wa mkoa wa Tanga  Martin Shigela , asisitiza maagizo ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli kwa  wakazi wa mkoa huo , ya kuendelea kuzingatia maagizo ya serikali  ikiwa ni pamoja na kutumia Dawa za asili ambazo huwa wanazitumia kwa ajili matatizo ya mafua kawaida ambayo pia inapatikana kwa urahisi.

Hayo ameyasema wakati akipokea masaada wa kiasi cha sh. Milioni 10 kutoka kwa kampuni ya JIANGXI GEO-ENGINEERING(GROUP)CORPORATION  ya kichina ambayo amekabidhiwa na  Mkurugenzi  wa kampuni hiyo  GM Mr. Chen Xianghuu  ambapo amesema ni kwa ajili ya kuunga mkono shughuli za Serikali za kupambana na maambukizi ya Ugonjwa wa Corona  ulioathiri ulimwengu pamoja na Tanzania kwa ujumla.

Shigela amasema kwamba Mkoa wa Tanga una misitu mingi na hivyo zipo Dawa za asili   zipo zingine zilizosajiliwa za zisizosajiliwa inayotokana na miti ambapo ni Tangawizi , Binzari , limau na  vitunguu saumu laikini pia kuzingati kukaa umbali wa mita  moja kutoka mwingine hadi mwingine.

Alisema kwamba wananchi wanaofanya biashara wakiwemo wale wanaofanya mshughuli za baa, kuendelea kuzingatia utaratibu uliowekwa wa kuzingatia maagizo ya serikali  na kuweza kuwashauri wateja wao kufuata maelekezo yalioweka na serikali ya kutokukumbatiana na kushikana na kwamba endapo itatokea wameshikana wanatakiwa kunawana mikono na sabuni  au kutumia  vitakasa mikono.

Alisema kuwa hakuna tiba ya ugonjwa Corona isipokuwa ni kuzingatia maagizo ya  serikali na wataalamu wa afaya  , na kuongeza kusema kuwa  pesa hizo walizopokea zitaingizwa kwenye  mfuko  maalumu wa  Covid 19 unaoratibiwa Waziri Mkuu ili kuweza kusaidia  kwenye janga la maambukizi ya ugonjwa huo.

Alisema  JGC kichina  ni kampuni inayojishugulisha na ujenzi hapa Tanzania , ambayo ina miradi mikubwa hapa Tanga imesaidia na kujenga wa Barabarabara,  wamejenga barabara ya Makorora, Msambwewni, Standi ya Kange  ambayo iko penmbeni ,na kujenga Dambo la  kuelkea mtimbwani hivyo wameamua kuunga mkono serikali katika mapambano ya COVID 19.

Kwa upande wake katibu  Tawala mkoa Tanga Judica Omari ameishukuru Kampuni hiyo kwa kutoa msaada huo kwani itasaidia katika kupambana na covid 19 kama ambavyo imekusudiwa naserikali kuunda mfuko maalum wa kuwekafedha za maafa ambapo fedha hizo zitaingizwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *