Kamishna wa Maadili asema mwitikio wa matamko ya Mali za viongozi ni yakuridhisha, huku matamko 366 yakiwasilishwa kimakosa

Kamishna wa Maadili Harold Msekela, amesema kwa asilimia kubwa tayari viongozi wa Serikali tayari wameshawasilisha matamko yao, huku akibainisha kuwa bado kunauelewa mdogo kwa baadhi wa watumishi kuwasilisha matamko wakati hawakutakiwa.

Akizungumza  na waandishi wa habari leo januari 9, 2020,  Nsekela amesema kuwa mawaziri, Manaibu waziri,Makatibu wakuu,viongozi wa vyombo vya Dola, Majaji , Wakuu wa mikoa  wote wamepeleka matamko yao wakiwepo Manaibu Katibu wakuu isipokuwa Naibu katibu mkuu mmoja ndiye hajawasilisha tamko lake.

“Hata mimi ninayeongea Kamishina wa Maadili ya Sekretalieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma nimewasilisha Tamkolangu la Rasilimali na Madeni ila mimi nawasilisha moja kwa moja kwa Rais msije kuniuliza kuwa mimi nawasilisha wapi”amesema Jaji Mstaafu Nsekela.

Ameongeza kuwa “Sisi tunashughulikia viongozi ,kwahiyo ukiniletea tamko wewe ambaye siyo kiongozi ni kukiuka kifungu cha sheria cha 9 (c) ambacho kinamtaka kila kiongozi ifikapo mwisho wa mwaka anatakiwa kuwasilisha matamko yake”amesema.

Amesema wamekuwa wamepokea matamko 366 ya watumishi ambayo hayakutakiwa kupelekwa katika ofisi hiyo na kuwataka watu kusoma sheria inayowaopaswa viongozi wa umma kuwasilisha matamko ili wale wanaostahili ndio watekeleze agizo hilo.

Kuhusu viongozi ambao wanachelewesha matamko yao  amesema kuwa kisheria hawajafanya kosa lolote la kimaadili kwani ni haki yao ingawa kwa upande wao inawapa presha kubwa pindi wawasilishaji wanapokuwa wengi kwa wakati mmoja.

“Sisi kazi yetu siyo kupokea tu hayo matamko bali lazima tuyaangalie kama limejazwa vizuri,na kama lina makosa basi tunamrudishia ili aweze kurekebisha makosa hayo” amesema.

Kuhusu taarifa za kuwepo kwa ,mwisho wa kupeleka matamko hayo Kamishina amesema kuwa ifikapo desemba 31 siyo mwisho wa kurejesha matamko bali atakaye peleka baada ya muda huo kupita lazima awe na barua inayoonyesha sababu za msingi za kuchelewesha kupeleka matamko hayo.

Akitoleo ufafanuzi kuhusu ucheleweshwaji wa matamko hayo Jaji Msitaafu Harold Nsekela amesema ni kutokana na umbali hadi kuzifikia Ofisi za Maadili za Kanda akitoleo mfano Kanda ya Nyanda za juu kusini.

“Ukiangalia mfano Kanda ya Nyanda za juu kusini inahudumia mikoa ya Mbeya, Njombe, Iringa,Rukwa na Katavi, lakini Ofisi zipo Mbeya kwahiyo watu Kama wa Mpanda lazima watume kwa Posta” amesema.

Pia amebainisha kuwa tangu Rais, Dkt John Magufuli kupeleka matamko yake sekretarieti  ya maadili ilisaidia kasi ya viongozi wote wa kitaifa kupeleka  matamko yao katika Ofisi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *