KAHAMA:Rais Magufuli azungumzia ujenzi wa Reli itakayounganisha Tanzania na Rwanda.

Tanzania na Rwanda zinakamilisha mchakato wa ujenzi wa reli itakayounganisha mataifa hayo mawili ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Reli hiyo itakayounganishwa na ile ya kati itaanzia bandari kavu ya Isaka wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.

Mradi huo ambao tayari hatua ya upembuzi yakinifu umekamilika utarahisisha usafirishaji wa mizigo kutoka bandari kavu ya Isaka kwenda nchi jirani.

Akizungumza na wananchi wa Isaka leo Rais wa JOHN POMBE MAGUFULI amesema kinachoendelea ni kutafuta fedha za utekelezaji.

Rais MAGUFULI amewataka wakazi wa Isaka kufanya kazi kwa bidii, hasa katika sekta ya kilimo na biashara ili kuzalisha mazao na bidhaa zitakazosafishwa kupitia miundombinu inayojengwa na Serikali.

Ametaja mahindi, mpunga na uwele kuwa miongonimwa mazao yanayoweza kuzalishwa kwa wingi na wakazi wa eneo hilo na mkoa wa shinyanga.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *