Jumuiya ya kiislamu ya Al Tijarah Al Rabiha ya Oman yajenga Zahanati ya kisasa Kahama.

Wito umetolewa kwa wananchi wilayani Kahama mkoani Shinyanga kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara ili kutambua maradhi yanayowasumbua na kupatiwa matibabu.

Hayo yamesemwa leo na Profesa Khalfan Al-Mandhari kutoka jumuiya ya Kiislamu ya Al Tijarah Al Rabiha nchini Oman wakati wa ufunguzi wa zahanati ya Mascut iliyopo mtaa Nyakato kata ya Nyasubi.

Profesa Khalfan amesema kuwa upatikaji wa Zahanati hiyo itasaidia jamii kupata huduma bila kujali itikadi ya dini wala makabila na kuitaka jamii kuitunza zahanati hiyo.

Akito shukrani kwa niaba ya wananchi Mtendaji wa kata ya Nyasubi Innocent Kapere ameishukuru taasisi hiyo kwa kujenga zahati hiyo na kwamba itasaidia kupunguza foleni katika hospitali ya wilaya ya Kahama.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Masjid Al-wahab Mohamed Alhabsy amewataka wananchi wa Kahama kuwa kitu kimoja katika kuitunza  zahanati hiyo ikiwa ni pamoja na kufika kutibiwa huku katibu wake Shehe Ahmed Al-Nuby akisema kuwa zahanati hiyo haibagui dini ya mtu.

Zahanati ya Mascut iliyopo Mtaa wa Nyakato kata Ya Nyasubi iliyozinduliwa leo imejengwa kwa ufadhili wa Jumuiya ya kislamu ya IAl Tijarah Al Rabiha nchini Oman na inatarajia kuanza kazi kuanzia jumatatu wiki ijayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *