Juma Duni ahofia mazingira uchaguzi mkuu ujao Zanzibar

Unguja. Naibu kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zanzibar Juma Duni Haji amesema ikiwa imesalia mwaka mmoja kufika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 chama hicho kinaona kuna kila aina ua ugumu kwenye uchaguzi huo kutokana na mazingira yaliowekwa.

Duni ameyasema hayo leo Jumapili Novemba 17, 2019 wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Unguja kuelezea miaka 9 ya utawala wa Rais Mohamed Shein.

Amesema kuna mazingira magumu ya uchaguzi ujao kwa kuwa wapo baadhi ya watu wameweka mbele  zaidi maslahi ya chama chao kuliko maslahi ya wananchi.

Hata hivyo, amesema kinachowafanya wawe na mashaka zaidi ni kuvunjwa kwa  mfumo mzima wa sheria ya uchaguzi na Tume ya uchaguzi Zanzibar ( ZEC) ilioweka wazi uwepo wa  wajumbe kutoka vyama vya upinzani na hilo halikufanyika katika awamu hii.

Pamoja na hayo Duni amesema ni pamoja na kuvunja dhamira ya kulinda umoja wa taifa Dk Shein ameteua tume yenye wajumbe takriban wote wastaafu na wakereketwa wa  CCM wenye kumbukumbu mbaya za kiutendaji dhidi ya upinzani walipokua serikalini.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *