Jeshi nchini Nigeria laanzisha operesheni dhidi ya wanmagambo wa Boko haramu

Kamanda mkuu wa jeshi la Nigeria Tukur Bı-uratai  amewaambia wanahabari kuwa  jeshi limeendesha  operesheni dhidi ya wanamgambo wa boko haramu katika jimbo la  Borna, Aamawa na Yobe karibu na ziwa Chad.

Operesheni katika eneo hilo imeendeshwa katika kipindi cha mweiz moja na nusu.

Katika kipindi cha wiki 6 zilizopita,  kamanda huyo amesema kuwa wanamgambo 1015  wa kundi la bok haramu wameangamizwa na wengine zaidi ya  100 wamejeruhiwa katika operesheni zilizoanzishwa na jeshi la Nigeria.

Wanamgambo 84 wamekamatwa na silaha zao  zimepokonywa .

Askari  11 wameuawa pia  katika operesheni hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *