Jeshi La Polisi Kanda Maalumu ya Dar Lafanikiwa Kumuua Jambazi Sugu

Polisi kanda Maalumu ya Dar es Salaam, wamefanikiwa kumuua jambazi maarufu aliyekuwa akitafutwa kwa muda mrefu anayejulikana kwa jina la Kambale, usiku wa kuamkia  Novemba 6, 2019, eneo la Ukonga Mazizini, jijini humo na kumkuta na silaha moja aina ya Bastola.
Taarifa hiyo imetolewa  Novemba 6, 2019, na Kamanda wa kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa imesema kuwa, jambazi huyo alikuwa ni maarufu sana kutokana na matukio yake ya utekaji wa bodaboda na kuwaua watu.

“Katika juhudi zetu za kupambana na uhalifu, tumeua jambazi maarufu sana alikuwa anaitwa kambale, ametesa sana kule Ukonga – Mazizini na Kinyerezi, amekuwa anateka watu na kuwaua bodaboda na kufanya chochote anachotaka na jina la Kambale lilikuwa na maana ya kila akitaka kukamatwa anateleza”, amesema SACP Mambosasa.

Akizungumzia hali ya usalama ndani ya Jiji hilo, Mambosasa amesema kuwa bado wanaendelea kuwasaka wale wote, wanaotaka kuleta taswira tofauti ili kabla hawajatimiza lengo lao wawafikie na Jiji liendelee kuwa salama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *