Jamii yatakiwa kutibu maji kwa matumizi ya nyumbani

JAMII imetakiwa kipindi hiki cha masika ya mvua zinazoendelaea kunyesha kutibu maji kwa kutumia dawa zilizodhibitishwa na wizara ya Afya ili kujikinga na magonjwa ya mlipuko.

Ushauri huu umetolewa na Afisa Afya na mratibu wa uelimishaji Afya wa halmashauri ya mji wa Tarime,Agrey Hyera wakati akiongea na waandishi wa Habari Ofisini kwake.

Agrey alisema kuwa kuna magonjwa ya mlipuko mengi nyakati za masika ya mvua kwa hali hiyo jamii inatakiwa kuchukua tahadhari ya kujikinga kama vile kuchamsha maji na kuyachuja kwa matumizi ya nyumbani.

“Mimi kama mtaalamu wa Afya niseme kuwa jamii inakumbwa na magonjwa ya mlipuko kutokana na kutozingatia taratibu na kanununi za Afya “alisema Agrey.

Afiisa huyo aliongeza kuwa wanawake au watu waliowengi wanachemsha maji kunywa ambapo pia hawachuji huku wakiamini kuwa hawatapatwa na magonjwa ya mulipuko hiyo haitoshi inatakiwa kwenda mabli zaidi na kuchemsha maji yote ya matumizi ya nyumbani ikiwa ni pamoja na yale ya kuonga aliongeza kusema.

Afisa huyo alitumia nafasi hiyo kushauri Watanzania kwa ujumla kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa wa CORONA hususani wale ambao wanaishi mipakani kama vile Tarime mpakani mwa nchi jirani ya Kenya huku wakijua kuwa ugonjwa huu bado unaendelea kuwatesa watu wa mataifa mengine tunayopakana.

Agrey alibainasha baadhi ya magonjwa ya mlipuko ambayo yanatokea kipindi cha mvua kuwa ni pamoja na kuhara,kipindupindi,magonjwa ya matumbo na ameeba na mangine mengi.

Mmoja wa wakazi wa mjini hapa Faustena Jumanne alibainisha kuwa wengi wa wananchi hapa Tarime wamejenga tamaduni ya kutumia maji ya mvua bila kuyatibu huku wakiamini kuwa yametoka kwa Mungu na nisalama na hayana madhara.

Jumanne aliongeza kusema kuwa bado elimu ya Afya haijawafikia waliowengi hususani juu ya matumizi sahihi ya maji kwa matumizi ya nyumbani ambapo alisema kuwa baadhi ya jamii inakunywa maji ya visima vya kuchimba ambayo hayatibiwi wala kuchemshwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *