Jamii imetakiwa kusimama katika misingi ya dini ili kuondokana na imani Potovu.

Jamii imeshauriwa kusimama katika misingi ya dini ili kuondokana na imani potofu ambazo hupelekea kupoteza mali nyingi pamoja na muda katika kufanya mambo yasiyofaa ambayo hupelekea kushuka kwa maadili ikiwemo kutokuwaheshimu wazazi pamoja na viongozi wa dini.
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa Masjid al wahab Sheikh MOHAMED ISSA AL HABSY wakati wa uzinduzi wa msikiti wa Chela katika kijiji cha CHela wilayani KAHAMA ambapo amesema nyumba za ibada zinasaidia jamii kuwa katika hali ya usalama na kuepukana na mambo yasiyofaa ikiwemo kamali ambayo ndiyo chanzo cha anasa.
SHEIKH MOHAMED amesema upo umuhimu mkubwa kwa jamii kufata misingi ya imani ambayo inaweza kuondokana na mifarakano pamoja na uadui ambapo ni miongoni mwa matendo yasiyofaa ndani ya jamii akitolea mfano mauaji ya albino.
Naye mwenyekiti wa kiijiji hicho ATHONY SHAGEMBE amesema waislamu wamekuwa ni watu wa kwanza kutengeneza nyumba nzuri ya kuabudia katika eneo hilo ambayo itasaidia wananchi kuacha kusafiri umbali mrefu kutafuta nyumba kwa ajili ya kuambudu ambazo zilikuwa ni changamoto kubwa katika kata hiyo.
Kwa upande wake YASNI ADAM SULEIMAN PAMOJA NA HAMIDA wameshukuru kuzinduliwa kwa msikiti huo ambao utasaidia waislam kusali kwa wakati ambapo kabla ya msikiti huo walikuwa wanalazimika kusafiri katika kijiji cha busangi kilichopo umbali wa kilometa 15 huku wanawake wakibaki kuswali majumbani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *