Jafo: Kamati za Rufaa Tendeni Haki kwa Wagombea

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amezitaka Kamati ya Rufaa za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kutenda haki wa wagombea wote watakaowasilisha malalamiko yao kuhusu uteuzi.

Waziri Jafo ameyasema hayo wakati akizungumza na Kamati ya Rufaa pamoja na viongozi wa Mkoa wa Manyara katika ziara yake Mkoani humo kuangalia maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, 2019, Tarehe 6/11/2019.

Amesema tunataka haya malalamiko yanayoendelea huko nje hivi sasa yaishe na kuisha kwake ni ninyi wajumbe wa Kamati  hii kufanya kazi yake kwa umakini na uadilifu mkubwa ili kuhakikisha haki inatendeka.

“Tunategemea sana Kamati hizi za Rufaa zilizoundwa katika kila Wilaya Nchini kote, katika kutenda haki na kuweka mambo yote sawa ili  kila mtu awe na amani na tukamilishe zoezi la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa” alisema Jafo.

Aliongeza kuwa katika mchakato huu musimuonee aibu yeyote na wala msimuonee au kumpendelea mtu katendeni haki kwa watu watakaoleta  malalamiko yao kwenu ili kila mtu afurahie Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na ukamalike kwa amani

Ndio maana mmechaguliwa kutoka Taasisi za Ummambalimbali na  hamkutoka katika ofisi moja kila mmoja wenu katoka kwenye Taasisi yake hii itasaidia kupunguza mgongano wa maslahi kwa kuwa ninyi wengi hamfanyi kazi katika Serikali za Mitaa.

“Pimeni malalamiko kwa weledi wenu na kufuata Kanuni toeni maamuzi stahiki, inawezekana kabisa kwa Kamati ya Rufaa ikamrudisha mtu kwenye nafasi yake mbayo aliyeunguliwa hapo awali mkiona anastahili kwa mujibu wa vielelezo alivyowasilisha mrejesheni hiyo ndio kazi yenu kubwa katika kamati hii” Alisema Jafo.

Aliongeza kuwa wagombea wote ambao kuna baadhi ya vitu wanaona havikwenda sawa huu ndio wakati sasa wa kuviwasilisha kwenu ili muweze kuhakiki na kufanya maamuzi ya busara yanayofuata utaratibu, sheria na maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni Uchaguzi wa Wananchi, ni vyema michakato yote ikafanyika kwa haki kwenye ngazi zote haswa hii ya kugombea nafasi za uongozi haki inatakiwa kuonekana imetendeka hivyo  Kamati ya Rufaa nawaelekeza fanyeni kazi hii kwa haki, mkijiamini na kutoa maamuzi yatakayomaliza malalamiko ya wagombea alimalizia Jafo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *