Jafo Akerwa Na Utendaji Kazi Wa Watumishi Manispaa Ya Shinyanga

Waziri wa nchi ofisi ya Rais,Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo amemwagiza katibu Mkuu wake TAMISEMI kuwahamisha vituo vya kazi Maafisa wawili wa Manispaa ya Shinyanga baada ya kubainika kufanya kazi kwa makundi hali ambayo inaweza kukwamisha shughuli za Umma.
Waziri Jafo amewataja maafisa hao kuwa ni pamoja na Ofisa utumishi wa manispaa ya Shinyanga, Magedi Magezi pamoja na Mweka hazina Paschal Makoye, wahamishwe na  kuwapelekwa katika katika vituo vingine vya kazi.
Jafo ametoa agizo hilo jana baada ya kupokea taarifa ya mkoa wa Shinyanga, kutoka kwa  mkuu wa mkoa wa shinyanga,  Zainab Telack, katika ziara yake ya kikazi ya siku moja iliyoenda sambamba  na ukaguzi wa  ujenzi wa hospitali halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
“Kuna tabia ya watumishi katika manispaa hii wanafanya kazi kwa  makundi na hakuna umoja hasa wakuu wa idara kila mtu ni  mtawala na kusababisha utendaji kazi mbovu nimeamua kuwaondoa ili wakafanya kazi katika sehemu nyingine kuliko kuliko kuwaacha wakiendelea kuwagawa watumishi”alisema Jafo.
Waziri Jafo amesema TAMISEMI itaendelea kufuatilia nyendo za watumisho wote  wa Halmshauri nchini ambao wanafanya kazi kwa mazoea ambao hawaendi na kasi ya Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dk John Pombe Magufuli kwa kuwachukilia hatua za kidhamu ikiwanipamoja ka kuwahamisha katika vituo vya kazi.
“Mimi niko hapa kumsaidia Mh,Rais na siwezi kukubali kuona watumishi wanafanya kazi kwa makundi,nimeshatoa maelekezo kwa wakuu wote wa idara kufanya kazi kwa kushirikiana ili ufanisi wa shughuli za serikali ziweze kufanikiwa na wananchi wapate huduma bora”alisema Jafo.
Katika hatua nyingine Waziri Jafo, amepongeza ujenzi wa hospitali halmashauri ya wilaya ya Shinyanga baada ya kuyakagua na kuridhika na ujenzi wake na kusema kuwa  Rais Dk John Magufuli amekubali kutoa  Shilingi Milioni 500 ziwezekutumika kuongeza majengo mengine.
Nae  mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, alibainisha kuwa  kuwa  Serikali ilitoa Shilingi, Bilioni 3 kwaajili ya kujengwa hospitali mbili za wilaya katika mkoani huo, katika Halmashauri za Ushetu na Shinyanga  ambazo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 90.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *