Ivory Coast inahofia kuwa na mgonjwa mwenye virusi vya corona

Mwanafunzi ambaye jina lake halikutajwa, alikuwa ametokea China, mjini Beijing na kurudi kwao Afrika magharibi siku ya jumamosi, sasa anafanyiwa vipimo zaidi baada ya kukutwa na mafua, ambayo ni moja ya dalili za ugonjwa wa corona.

Imethibitishwa kwamba mgonjwa huyo atakuwa wa kwanza barani Afrika kufanyiwa vipimo hivyo vya virusi hatari.

Virusi hivyo vilibainika kwa mara ya kwanza katika mji wa China wa Wuhan, na sasa watu 2000 wana virusi hivyo na 56 wamefariki tayrari.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 34, ametengwa kwa sasa, maofisa walisema.

Mwanamke mhuyo anadaiwa kuishi China kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, kwa mujibu wa taarifa ambayo ilitolewa na wizara ya afya ya Ivory Coast na kusema kuwa alionyesha dalili za mafua kabla hajapanda ndege akiwa anaelekea Abidjan.

“Kuna hali ya wasiwasi kuwa dalili alizokuwa nazo zina uhusiano na virusi vya corona.”

Majibu ya vipimo vya mwanamke huyo yanatarajiwa kutolewa siku ya jumapili jioni.

Kwa sasa virusi hivi vinavyofahamika kama 2019-nCoV, vinadaiwa kuwa maambukizi mapya kuwapata binadamu.

Tangu mlipuko wa ugonjwa huo kuanza Wuhan, mataifa kadhaa ya Afrika yalianzisha vipimo vya kuangalia virusi vya corona kwa wat wanaotoka China.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *