Hussein Mwinyi na Maalim Seif wapiga kura Zanzibar

Wagombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Hussein Mwinyi na Chama cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad, tayari wamepiga kura hii leo visiwani humo, huku kila mmoja wao akiwaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kupiga kura.

“Nawapongeza Wanzanzibar wote ambao wametumia haki yao ya kupiga kura na niwaombe ambao hawajafika waendelee kujitokeza kupiga kura na hatimaye zoezi liishe kwa amani” Dkt Mwinyi

Kwa upande wake mgombea urais kupitia chama cha ACT Wazalendo, Maalim Seif amesema kuwa masuala ya kuwatoa mawakala katika vituo siyo sahihi kwani wakala anakuwepo mahala pale kwa lengo la kulinda kura za mgombea wake

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *