Hatimaye Kinana amuomba msamaha Rais Magufuli.

Baada ya kimya cha muda mrefu hatimaye katibu mkuu mstaafu wa chama cha mapinduzi Comrade Abdulrahaman Kinana amejitokeza hadharani na kumuomba radhi Mwenyekiti wa Chama ChaMapinduzi taifa Dkt. John Pombe Magufuli kwa matukio mbalimbali yaliyojitokeza baada ya kung’atuka katika uongozi chama hicho.
Kinana pia amewaomba radhi Watanzania na wanachama wa CCM aliowakwaza kwa kitendo kilichotokea.
Awali akizungumzia adhabu aliyopewa na Chama Kinana amekiri kutokea kwa jambo hilo na kudai kuwa kama binadamu alighafilika na kudai kuwa akiwa ni mkongwe katika chama hicho adhabu ni utaratibu uliopo katika chama chochote kwa kiongozi au mwanachama anapokosea.
Wakati huo huo Komrade Kinana ametembea ofisi za CCM mkoa wa Arusha na kuzungumza na mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Arusha Zelothe Stephen Zelothe.
Kinana akiwa na baadhi ya viongozi wakongwe wa chama hicho walipewa adhabu hiyo baada ya mazungumzo yao ya simu kunaswa wakimteta rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na kusambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii hali iliyosababisha uongozi wa CCM kuwaita na kuwahoji, viongozi hao wakiwemo wastaafu na waliopo madarakani.
Tangu sakata hilo litokee Katibu mkuu huyo mstaafu wa CCM Abdulrahamani Kinana hakuwahi kusikika katika vyombo vya habari wala mitandao ya kijamii kuzungumzia sakata hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *