Ghasia zapungua katika maandamano ya kupinga mauaji ya George Floyd huko Marekani

Maandamano yaliyofanyika usiku wa kuamkia leo nchini Marekani kufuatia kifo cha George Floyd akiwa mikononi mwa polisi, yalikuwa ya amani ila kumesambaa video iliyolaaniwa mno mtandaoni ambapo afisa mmoja wa polisi anaonekana akimsukuma mtu mmoja mwenye umri wa miaka 75 ambaye aliangukia kisogo na kuanza kuchurizika damu.

Meya wa mji wa New York, Byron Brown amesema video hiyo imemvuruga akili sana na akasema mtu huyo kwa sasa yuko katika hali mbaya ila anatarajiwa kupona.

Mkuu wa polisi mjini humo amewasimamisha kazi bila malipo maafisa wawili waliohusika katika tukio hilo.

Haya yanatokea wakati ambapo George Floyd alifanyiwa misa ya wafu hapo jana iliyohudhuriwa na maelfu ya watu miongoni mwao wakiwa wanamuziki mashuhuri nchini Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *