George Floyd kuzikwa leo, Maelfu wajitokeza Houston kutoa heshima za mwisho

George Floyd, Mmarekani mweusi mwenye umri wa miaka 46 ambaye mauaji yake na polisi mweupe yamembadilisha kuwa picha ya ulimwengu ya mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi na ukatili wa polisi, atazikwa leo mjini Houston, ambako alikulia. Maelfu ya watu walijitokeza kutoa heshima zao mjini Houston jimbo la Texas.

Jeneza lake lililokuwa wazi lilipelekwa katika kanisa la The Fountain of Praise ambapo karibu watu 6,000 walifika kumuaga. Mgombea wa urais wa chama cha Democratic Joe Biden, alikutana na wanafamilia ya Floyd.

Atazikwa leo kando ya kaburi la mamake katika hafla ya faragha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *