Freeman Mbowe Alazwa Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam

Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, Freeman Mbowe, ameshindwa kufika mahakamani kutokana na kulazwa katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam akiwa anapatiwa matibabu.
Mbowe aliyelazwa  tangu  Novemba 17, 2019b ni miongoni mwa viongozi tisa wa CHADEMA wanaokabiliwa na kesi ya uchochezi namba 112/2018 inayoendelea leo Jumanne Novemba 19, 2019  na alitakiwa kuendelea kujitetea leo lakini mdhamini wake,  Greyson Selestine ameieleza mahakama  kuwa anaumwa.

Kinachoendelea kwa sasa Mahakamani ni washtakiwa wanne; John Heche; Ester Bulaya, Mchungaji Peter Msigwa na Halima Mdee  kujitetea kwanini wasifutiwe dhamana.

Novemba 15, 2019, mahakama hiyo ilitoa amri ya kukamatwa kwa washtakiwa hao kutokana na kukiuka masharti ya dhamana baada ya kutofika  mahakama kusikiliza kesi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *