Familia ya kifalme yajadili suala la mwanamfalme Harry na Meghan

Mwanamfalme Harry na mwanamfalme William wamekanusa taarifa ya uongo iliyoandikwa katika gazeti la Uingereza kuhusu mahusiano yao.

Maelezo yaliyotolewa kwa niaba ya mwanamfalme Harry na William ameelezea taarifa hiyo kuwa ya kizushi na iliyotumia lugha ya kichochezi.

Taarifa hiyo imekuja baada ya chanzo cha taarifa kuliambia gazeti la Times kuwa mwanamfalme Harry alipata msukumo wa kuondoka katika shughuli za kifalme kutokana na tabia za unyanyasaji za William.

Ndugu hawa watakutana na malkia pamoja na wakuu wa familia kifalme huko Sandringham kujadili majukumu ya baadae ya mwanamfalme Harry na mkewe Meghan.

Mwanamfalme Harry, kaka yake mwanamfalme William na baba yao mwanamfalme Charles watahudhuria kikao hicho, huku Meghan anatarajiwa kujumuika kwa njia ya simu akiwa Canada.

Mwanamfalme Harry na mkewe wanapanga kujihudhuru na majukumuku ya kifalme.

Mwandishi wa masuala ya kifalme wa BBC, Jonny Dymond ameelezea mkutano huo kuwa ni mkutano wa kihistoria katika familia ya kifalme.

Kikao hicho kinaleta matumaini kuwa mazungumzo hayo yataweza kuwapa mwanya wapenzi hao wapya katika familia ya kifalme kupiga hatua na vilevile malkia kupata suluhu kuhusu suala lao.

Hata hivyo mwandishi wetu alisema kuwa majadiliano hayo yatachukua muda kufikia makubaliano na kuanza kufanyiwa kazi.

Miongoni mwa masuala ambayo yanatarajiwa kuzungumzwa ni namna mwanamfalme Harry na mkewe wataweza kupata ufadhili, na kama wataendelea kubaki na wadhifa wao wa kifalme au la.

Malkia ,mwanamfalme Charles, William na Harry wanatarajiwa kuhakiki majukumu yao ya kifalme na kupanga jinsi shughuli za kifalme zitaweza kuendelea bila uwepo wa mwanamfalme Harry na mkewe.

Leo hii itakuwa ni ya kwanza kwa malkia kufanya mazungumzo na mwanamfalme Harry na mkewe tangu watangazwe nia yao.

Mwanamfalmee Charles amerejea kutoka Oman ambapo alihudhuria mazishi ya sultani Qaboos.

Magazeti yameripoti kupendekeza wapenzi hao kuweza kufanya mahojiano ya televisheni , kama watakuwa hawajafurahia matokeo ya majadiliano hayo.

Mtangazaji na rafiki wa wapenzi hao, Tom Bradby – aliyefanya makala kuhusu wao mwaka jana – aliandika katika gazeti la Sunday Times: “Nina wazo la nini kinachoweza kutangazwa kwa ujumla, sidhani kama kukaa kufanya majuano ni jambo zuri kwa sasa.”

Huko Sandringham hapo baadae wataweza kuchagua namna nzuri.

Hii itazingatia na malengo ya mwanamfalme Harry na mkewe Meghan.

Ukiachilia mbali mkanganyiko huu, maelezo ya zaidi yanahitajika , ili kuweza kuweka usawa katika malengo yao ambayo yanaleta utofauti na kuonekana kuwa wanaomba jambo gumu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *