Dr Mataba: Waandishi wa Habari heshimuni haki na mipaka katika kazi zenu.

ARUSHA

Waandishi wa habari nchini wametakiwa kuheshimu haki za watu wengine pamoja na kuzingatia mipaka pindi wanapotimiza uhuru wao wa kutafuta na kutoa habari.

Wito huo umetolewa jijiji Arusha na Mhadhiri wa chuo kikuu cha SAUT Mwanza Dr.Petet Mataba katika semina ya mafunzo ya habari za uchunguzi na matumizi ya Tehema iliyoandaliwa na Shirika la Kimataifa la Elimu,Sayansi na Utamaduni (UNESCO)

Mataba amesema kuwa licha ya kwamba waandishi wa habari wana uhuru wa kutafuta na kukusanya habari wanao wajibu wa kuheshimu haki za watu pamoja ya kutovuka mipaka katika maeneo ambayo hawaruhusiwi kufika.

Ameongeza kuwa faragha ya mtu ni muhimu kuheshimiwa na kwamba ikiwa jambo lina maslahi kwa jamii wafuate maadili ya uandishi wa habari ikiwa ni pamoja na kuzingatia kanuni za uandishi wa habari.

Kwa upande wao Anastazia Muganyizi kutoka Redio Uvinza na Masood Jongo kutoka Radio Rwangwa wamesema kuwa ushauri uliotolewa na Dr.Mataba umewaongezea weledi katika jukumu lao la kutafuta habari na kwamba elimu waliyoipata wataenda kuwashirikisha wenzao katika vituo vyao.

Mafunzo hayo ya siku Sita yaliyoandaliwa na Shirika la kimataifa la Elimu,Sayansi na utamaduni (UNESCO) yameshirikisha Radio 27 za kijamii kutoka Tanzania bara na Zanzibar ikiwemo Redio Kahama Fm ya Wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *