Dkt. Magufuli kuapisha leo kuwa rais kwa awamu ya pili

Rais Magufuli ameibuka kidedea katika uchaguzi mkuu ukiofanyika wiki iliyopita na kujizolea ushindi wa asilimia 84.4 na kuwashinda wapinzani wake 14 kutoka vyama mbalimbali vya upinzani.
Kwa mara ya kwanza jiji la Dodoma linashuhudia kufanyika kwa sherehe za kuapishwa kwa rais.

Kuanzia saa kumi na mbili asubuhi milango ya uwanja wa Jamhuri ilikuwa wazi kwa ajili wa wananchi waliofurika kutoka maeneo mbalimbali ya nchi.

Viongozi mbalimbali kutoka nchi zaidi ya 12 huku wawakilishi kutoka jumuiya kama vile SADC na AU wakitarajiwa kuhudhuria.

Rais Magufuli anaanza kuwatumikia Watanzania katika kipindi cha pili cha uongozi wake baada ya kutangazwa mshindi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *