Vijana mbalimbali wanaoshiriki mafunzo ya jeshi la akiba eneo la Old Shinyanga manispaa hiyo wakiwa katika gwaride wakati mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko alipokuwa akiangalia ukakamavu wa vijana hao.
Vijana 149 toka Manispaa ya Shinyanga wamejiunga na mafunzo ya jeshi la akiba ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha wanadumisha amani, umoja na ulinzi wa nchi katika maeneo yao pamoja na kujiimarisha kiafya .
Akifungua mafunzo hayo Agasti 25 Old Shinyanga, Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mh Jasinta Mboneko amewaasa vijana hao kuyatumia vema mafunzo hayo ya kijeshi yanayotolewa na Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuhakikisha wanalinda na kudumisha amani ya nchi pamoja na kujenga mshikamano na umoja
Mboneko amesema kuwa mafunzo hayo ambayo kwa sasa yamefikisha wiki 7 toka kuanza kwake huku yakitarajia kuchukua miezi minne ambapo amewataka kuwa na nidhamu wakati wote wa mafunzo na kuacha kusua kusua kwenye mafunzo.
“Kwa hiyo hakikisheni mnahudhuria mafunzo kila siku lakini nidhamu iwe ya hali ya juu mpo kwenye mafunzo tunatizama vitu kuna mnatakavyojifunza darasani na vingine huku na kila siku nitakuwa napewa taarifa juu ya mafunzo haya kwa hiyo kikubwa ni kuzingatia na kushika maelekezo mnayopewa na wakufunzi wenu”amesema Mboneko
Dc Mboneko ameongeza kuwa kwa sasa nchi inaelekea kwenye uchaguzi mkuu ambapo suala la amani linapaswa kudumishwa ambapo amewaasa kuendlea kutunza nidhamu na utulivu pamoja na kutoa taarifa za hali ya uvunjifu wa amani kwenye maeneo wanakotoka
“Kikubwa ni kuhakikisha kwamba maeneo yetu tunakotoka na kusihi mnakuwa na ninyi ni jicho la serikali na hapa nimeambiwa mko 149 nategemea mmalize wote kwa hiyo niwatahadhirishe msijiingize kwenye vikundi vya kuhatarisha amani mkono wa sheria utachukua nafasi yake”ameongeza Mboneko
Naye Mkuu wa mafunzo hayo Kanali Prosper Masawe toka base ya Shinyanga amesema kuwa jukumu la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ni kutoa mafunzo kwa lengo la kusaidia ulinzi kwenye maeneo wanayotoka pamoja na kuimarisha ulinzi wa nchi hususani nchi inapoingia kwenye vita huwa tunawatumia katika mapigano.
“Tunawasihi wale Vijana ambao wako mtaani asijali umri wala elimu kama hajapata mafunzo ya ulinzi wa nchi yake ni vizuri aje kwenye mafunzo haya ya Jeshi la akiba ambayo tunatumia miezi minne anakuwa tayari ameelewa kwa hiyo hii ni hatua ya nne watakwenda hadi hatua ya kwanza”amesema Kanali Masawe
Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakiwemo Vijana ambao ni watumishi wa serikali toka Manispaa ya Shinyanga wamesema kuwa jukumu la ulinzi wa nchi ni la kila mtanzania hivyo mafunzo hayo yatawasaidia katika kupamabana na vitendo vya uharifu kwenye maeneo yao
Ezra Majerenga ni Afisa Maliasili na Mazingira Manispaa ya Shinyanga anayeshiriki kwenyemafunzo hayo amesema kuwa katika kuimarisha ulinzi wa rasimali za nchi lazima uwe na utayari na ukakamvu wa mwili.
“Ili uweze kuwa mlinzi mzuri wa rasilimali za nchi unastahili kuwamkakavu na unahitaji mbinu za medani kwa maana ya kujua wapi ambapo maliasili zinatumka vibaya na mifumo ya kuhakiisha kwamba unazilinda kwa kusimamia sheria na taratibu zilizopo” amesema Ezra
Ufunguzi huo umeambatana na upigaji wa Shabaha kwa askari hao wa Jeshi la akiba,viongozi wa serikali wakiongozwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa uimarishaji wa suala la ulinzi wa nchi.
CREDIT: Shinyanga Press Club