DC Jokate Mwegelo Kasema Kisarawe Imeanza Kuzalisha PPE, barakoa na vitakasa mikono Kwa Ajili Ya Kukabiliana na Corona

Hospitali Ya Wilaya Ya Kisarawe katika kuwalinda wahudumu wote wa afya waliomstari wa mbele katika mapambano ya Virusi vya Corona, imeanza kuzalisha PPE

Pamoja na hayo pia imeanza kuzalisha barakoa na vitakasa mikono vyote tayari vinapatikana kwenye famasia/pharmacy wilayani humo.

Hayo yameelezwa Leo Ijumaa May 08, 2020 na Mkuu wa Wilaya hiyo, Jokate Mwegelo kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Akizungumzia ubora wa vazi hilo ambalo linafanana na lile linalozalishwa Muhimbili, Jokate ameandika; “Kuhusiana na ubora wa vazi letu la PPE; Quality ni kama ile ya Muhimbili kwa maana ya material iliyotumika lakini kwa maana ya uimara yetu imeongezwa uimara wa ndani kuzuia isichanike/kutatuka haraka wakati wa kuitumia.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *