DAVID KISSU WA AZAM FC AWEKA REKODI YAKE BONGO

DAVID Kissu Mapigano kipa namba moja wa Azam FC ameweka rekodi ya kuwa kinara wa clean sheet ndani ya Ligi Kuu Bara Bara msimu wa 2020/21 akitumia dakika 540 bila kuruhusu kufungwa na kumpoteza Daniel Mgore kipa wa Biashara United.
Kissu ambaye ni ingizo jipya kutoka Klabu ya Gormahia ya Kenya ameweza kukaa langoni kwenye mechi saba na ametunguliwa mechi moja mabao mawili wakati timu yake ya Azam FC ikishinda mabao 4-2 dhidi ya Kagera Sugar.

Daniel Mgore wa Biashara United kweneye mechi saba alizokaa langoni ameruhusu kufungwa kwenye mechi mbili, ilikuwa ni mbele ya Simba wakati ikifungwa mabao 4-0 na mbele ya Coastal Union wakati ikipoteza kwa kufungwa mabao 3-0.

Mgore ana clean sheet tano ndani ya ligi kwa msimu wa 2020/21 na msimu uliopita alikusanya clean 18 na aliingia kwenye kinyang’anyiro cha tuzo ya kipa bora iliyochukuliwa na Aishi Manula wa Simba mwenye clean sheet tatu kwenye mechi tano alizocheza.

Mechi ambazo hajafungwa Kissu ilikuwa ni mbele ya Polisi Tanzania wakati Azam FC ikishinda bao 1-0, Azam 2-0 Coastal Union, Azam 3-0 Mwadui FC ilikuwa ni Uwanja wa Azam Complex na Mbeya City 0-1 Azam, Ihefu 0-2 Azam FC,zote zilichezwa Uwanja wa Sokoine, Tanzania Prisons 0-1 Azam Uwanja wa Nelson Mandela.

Vivien Bahati, Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa kazi anayofanya Kissu inaonekana na hapaswi pongezi peke yake bali ni kazi ya timu na anapaswa kuendelea kuilinda rekodi hiyo.

Azam FC Kibindoni ina jumla ya pointi 21 na imefunga mabao 14 baada ya kucheza mechi zake 7. Imeweka rekodi ya kushinda mechi saba mfululizo ndani ya msimu wa 2020/21 ambazo ni dakika 630.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *