Daimond kuwalipia kodi za nyumba kaya 500, ataja utaratibu

Staa wa muziki nchini Nasibu Abdul maarufu kama Diamond Platnumz, amesema kuwa atachangia ‘kodi ya pango’ kwa kaya 500 nchini kwa ajili ya kupunguza makali ya kiuchumi kwa Watanzania katika kipindi hiki cha janga la corona

Leo katika mahojiano na wasafi FM amesema kuwa ameguswa na hali ya sasa na njia moja ya kuunga jitihada za Rais Magufuli kwakuwa watu wamekwama kwenye biashara zao na suala la kodi ni changamoto kubwa kwa watu wengi.

“Najua katika kipindi hiki cha Corona, mambo mengi hayajakaa sawa, hususani upande wa biashara, nyingi zimeshuka na kupelekea hali ya kifedha kuyumba na mambo kuwa kidogo magumu kwa wengi wetu… na mimi ni miongoni mwa walio ndani ya janga hili” alisema daimond.

Daimond aliendelea kusema kuwa wamejipanga ili kuhakikisha figisu hazitakuwepo na tutatumia serikali za mitaa pamoja na timu yetu ambayo itapita mitaani ili kuwafikia walengwa kama wamama wajane, walemavu na wale wote wenye mahitaji kweli na kila mkoa sitaenda katika familia tazo na asilimia kubwa itakuwa hapa Dar es salaam.

“Misukumo ya kusaidia watu , imetokana na malezi niliyolelewa, maisha niliyotokea na historia yangu ya nyuma. Nikikumbuka shida nilizopitia , napata Moyo wa kusaidia Wengine ”

Kuhusu kiwango kipi cha kodi atakacholipia daimond amesema kuwa inategemea kwakuwa mwanzo mwingine alikuwa anaweza kulipa laki laki mbili kwa mwezi lakini kwa sasa amekwama kweli huyo ni lazima asaidiwe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *