Benki ya CRDB kanda ya Magharibi yatoa Semina kwa mawakala wake wote mkoa wa Geita.

Benki ya CRDB kanda ya Magharibi imewapa mafunzo mawakala wake wote wa mkoa wa Geita jinsi ya kufanya kazi kwa ufanisi,Usalama na kufuata sheria za kibenki.

Mafunzo hayo yaliyofanyika jana mkaoni Geita yamejumuisha zaidi ya mawakala kutoka wilaya zote za mkoa wa Geita.

Akifungua Mafunzo hayo Mkuu wa Mkoa wa Geita Eng. Robert Luhumbi amesema kuwa benki ya CRDB imewasaidia wajasiliamali wengi na kupata mafanikio makubwa na kuwataka mawakala hao waendelee kufanya kazi kwa kufaata taratibu na sheria ili wajipatie kipato cha halali na cha uhakika.

Sambamba na hayo Eng Luhumbi amewahakikishia Mawakala wote wa Mkoa wa Geita kuwa hali ya usalama ni nzuri na kwamba  wafanye kazi kwa amani bila ya kuwa na hofu.

Kwa upande wake meneja biashara wa Benki ya CRDB kanda ya Magharibi Jumanne Wagana amewataka Mawakala kufika katika tawi lolote la benki hiyo wanapopata shida ili waweze kusaidiwa na kuendelea kutoa huduma bora za kifedha.

Wagana ameongeza kuwa Benki ya CRDB bado ina fursa nyingi na kutoa wito kwa wafanyabiashara wanaotaka kuwa mawakala kufika katika tawi lolote ili kujua utaratibu wa namna ya kuwa wakala wa benki hiyo.

Benki ya CRDB Kanda ya magharibi inayojumuisha mikoa ya Shinyanga,Tabora,Kigoma,Geita na wilaya ya Sengerema ina jumla ya mawakala 1,098 wanaotoa huduma za kifedha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *