CLATOUS CHAMA AITWA TIMU YA TAIFA YA ZAMBIA

NYOTA wa Klabu ya Simba, Clatous Chama ameitwa kwenye timu ya Taifa ya Zambia ili akaitumike timu yake hiyo maarufu kama Chipolopolo.

Kwa sasa timu ya Zambia ipo kwenye maandalizi ya mchezo wa kufuzu Afcon ambapo itamenyana na Botswana, Novemba 12 nchini Zambia.

Kiungo huyo ambaye amekuwa kwenye ubora ndani ya Bongo kwa msimu wa 2020/21 akiwa na pasi tano za mabao pamoja na kufunga mabao mawili ameitwa baada ya Enock Mwepu kuwa ‘locdown’.

Kiungo huyo anatumika ndani ya Klabu ya Red Bull Salzburg kutokana na wachezaji wa timu hiyo sita kukutwa na maambukizi ya Virusi vya Corona.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *