China yatoa msaada kwa Afrika katika kupambana na COVID-19

Awamu mpya ya vifaa vya matibabu iliyotolewa na China kwa nchi na sehemu 12 za Afrika kuzisaidia kupambana na virusi vya Corona imewasili jana katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa kupitia ndege ya mizigo ya Shirika la Ndege la Ethiopia.

Maofisa wa ngazi ya juu na wawakilishi wa kitaifa na kimataifa pamoja na wanadiplomasia na wawakilishi wa Umoja wa Afrika na Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa cha Afrika walishuhudia kuwasili kwa msaada huo.

Msaada huo umejumuisha vifaa mbalimbali vya matibabu ikiwemo mask, nguo za kujikinga, miwani za kujikinga, glovu na vifaa vya kufunika viatu kwa ajili ya matumizi ya kidaktari. Vifaa hivyo vinatarajiwa kupelekwa kwenye nchi na sehemu 12 za Afrika ikiwemo Zanzibar, Namibia, Lesotho, Angola na Somalia.

Kwa niaba ya nchi zinazosaidiwa pamoja na Umoja wa Afrika, balozi wa Lesotho nchini Ethiopia Marfa ameishukuru China kwa kutoa msaada huo muhimu. Amesema China siku zote inafuatilia hali ya maambukizi ya virusi vya Corona barani Afrika, na kuwa mbele zaidi katika kuzisaidia nchi za bara hilo kukabiliana na virusi hivyo. Ameongeza kuwa kutokana na miaada ya China na nchi nyingine za kirafiki, nchi za Afrika zimeimarisha imani na uwezo wa kukabiliana na maambukizi ya virusi hiyo.

Wakati huohuo, takwimu zilizotolewa na Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa cha Afrika zimeonyesha kuwa, idadi ya watu waliofariki kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona imefikia 1,242, huku idadi ya kesi zilizothibitishwa kuwa na maambukizi zikifikia 25,937 mpaka jana mchana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *