China yatangaza visa vipya 17 vya virusi vilivyoathiri zaidi ya watu 60

Mamlaka nchini China zimetangaza hii leo visa vipya 17 vya virusi vibaya kabisa vilivyoathiri zaidi ya watu 60 katika mji wa Wuhan.

Tume ya afya ya manispaa ya Wuhan imesema takriban watu watatu miongoni mwao wako katika hali mbaya na wawili wamefariki dunia.

Maafisa wa afya ya umma pamoja na shirika la afya ulimwenguni, WHO wameelezea virusi hivyo kama aina mpya ya jamii inayofahamika katika sayansi ya tiba kama Corona, ambavyo husambazwa kwa kukohoa, kupiga chafya na kugusana na mtu aliyeathirika na vinavyoweza kusababisha maradhi kuanzia mafua hadi homa ya mapafu.

Mamlaka za China Bara, Hong Kong na kwingineko zimeimarisha upimaji wa joto la mwili kwenye viwanja vya ndege katika jaribio la kuzuia virusi hivyo kusambaa zaidi.

Hadi sasa visa viwili vimeripotiwa Thailand na kimoja nchini Japan

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *