China yaionya Uingereza kwa kujitolea kuwapokea raia wa HongKong

China imeionya Uingereza kuingilia masuala ya Hong Kong baada ya taifa hilo kuapa kuwafungulia milango raia wapatao milioni tatu wa HongKong ambao wataondoka endapo sheria ya usalama wa taifa itapitishwa katika jimbo hilo.

Hatua ambayo China imesema haitakuwa na matokeo chanya.

Marekani na Uingereza zimekuwa zikiikosoa hatua hiyo ya China ambayo inawatia wasiwasi wachambuzi wengi wa kisiasa kuhusu mustakabali wa watu wa HongKong.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *