China inakaribisha juhudi za kutambua chanzo cha virusi vya corona

Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi amesema taifa hilo liko wazi kushirikiana na jamii ya Kimataifa ili kutambua chanzo cha mripuko wa virusi vya corona lakini ametahadharisha kuwa uchunguzi ufanyike bila kuingiliwa kati kisiasa.

Wangi Yi ameifokea Marekani kwa kile alichokiita juhudi za wanasiasa wa taifa hilo kueneza uvumi kuhusu chanzo cha mripuko huo na kutaka kuinyanyapaa China.

Yi amesema hali hiyo inaweza kusababisha nchi hizo kurejea tena katika enzi za vita baridi. Marekani na Australia katika wiki za hivi karibuni zimetaka kufanyika uchunguzi kamili juu ya chimbuko hasa la virusi hivyo.

Rais wa Marekani Donald Trump pamoja na Waziri wake wa mambo ya kigeni Mike Pompeo wameishutumu China kwa kutokuwa wazi kuhusu virusi hivyo, na mara kadhaa wamerejelea semi zao kwamba virusi vya corona vimetoka katika maabara ya China.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *