CHAUMA Nao Watangaza Kutoshiriki Uchaguzi Serikali Za Mitaa

Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA) nacho kimetangaza kutoshiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019.
Kimetangaza uamuzi huo siku mbili baada ya Chadema na ACT-Wazalendo navyo kutangaza kutoshiriki uchaguzi huo.
Mwenyekiti wa chama hicho, Hashim Rungwe ametangaza uamuzi huo leo Jumamosi Novemba 9, 2019 akibainisha kuwa wagombea zaidi ya 250 wa chama hicho wameenguliwa bila sababu za msingi.
“Haiwezekani nchi nzima wanaokosea kujaza fomu ni watu wa upinzani tu,  na sisi tumeamua kuwa hatutashiriki uchaguzi huu.Tunaomba wagombea wetu nchi nzima wasishiriki ” amesema Rungwe.
Rungwe alitumia nafasi hiyo kuwataka wanachama wake kutulia na kuachana na masuala ya uchaguzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *