CHAMA KUIKOSA YANGA UWANJA WA MKAPA KESHO

MAMBO ni mazito kwa mabingwa watetezi Simba ambao kesho wanakutana na Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Mkapa na huenda kesho wakakosa jumla huduma ya mtambo wao wa mabao Clatous Chama.

Simba ikiwa imefunga mabao 21 Chama amehusika kwenye mabao saba ambapo ametoa pasi tano za mabao na kutupia mabao mawili.

Kwenye mechi mbili ambazo hakuwepo kikosi cha kwanza wala benchi, Simba iliambulia maumivu kwa kupoteza pointi sita na kufungwa jumla ya mabao mawili ndani ya dakika 180.

Ilifungwa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons Uwanja wa Nelson Mandela na ikachapwa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa Uhuru.

Kwa mujibu wa Sven Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba, amesema kuwa maandalizi yapo sawa ila atakosa huduma ya Chama kwa kuwa ni majeruhi.

Kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Kagera Sugar Chama hakumaliza dakika 90 alitoka na kumpisha Miraj Athuman dakika ya 69.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *